23 Juni 2020 - 11:33
Mousavi: Azimio la haki za binadamu dhidi ya Iran limepasishwa kwa malengo ya kisiasa

Msemajii wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekutaja kupasishwa azimio kuhusu hali ya haki za binadamu dhidi ya Iran kuwa kumetegemea mitazamo ya kichochezi na inayogongana. Amesema azimio hilo lina malengo ya kisiasa.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sayyid Abbas Mousavi amelaani kitendo cha kupasishwa azimio hilo dhidi ya Iran katika kikao cha 43 cha Baraza la Haki za Binadamu na kusisitiza kuwa: Mienendo ya kindumakuwili na kutumia vibaya mifumo ya Umoja wa Mataifa vinawafedhehesha waungaji mkono wa azimio hilo. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kutumia kisiasa na kama wenzo suala la haki za binadamu na vigezo vya undumakuwili katika uwanja huo vinaelekea kuwa jambo la kawaida. Amesema, misimamo ya nchi hizo mkabala na ukandamizaji unaofanywa dhidi ya waandamanaji wanaopinga ubaguzi wa rangi huko Marekani, ni mfano mzuri wa kutathmini na kupima mienendo ya kundi la nchi hizo kuhusu haki za binadamu.  

Mousavi ameeleza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mfumo wa demokrasia ya kidini na kwamba Iran imechukua hatua ya kustawisha na kuboresha hali ya haki za binadamu kitaifa, kikanda na kimataifa katika fremu ya kuheshimu thamani za kidini, katiba sheria zingine na mikataba ya kimataifa ina inahakikisha kwamba inaheshimu kivitendo masuala hayo. 

Nchi wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa katika kikao chao cha 43 zimepasisha azimio kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Iran ambalo lilitayarishwa na Sweden ikisaidiwa na baadhi ya nchi za Magharibi. 


342/