29 Juni 2020 - 15:35
Merkel: Hatari ya maambukizi ya virusi vya corona ni changamoto kuu

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel amesisitiza udharura wa kudumishwa mapambano makali dhidi ya virusi vya corona na kuwataka wananchi wa nchi hiyo kutilia maanani vita vya kukabiliana na maambukizi ya virusi hivyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Angela Merkel amesema kuwa hatari ya maambukizi ya virusi vya corona bado ni changamoto kuu na kwamba wananchi wote wa Ujerumani wanawajibika kuchukua hatua za kukabiliana na maambukizi ya virusi hivyo. Kansela wa Ujerumani amewataka Wajerumani kutekeleza sheria za  kipindi cha maambukizi ya corona la ikiwa ni pamoja na kutumia barakoa (mask) katika maeneo ya umma na kusafisha mikono ili kujikinga na maambukizi ya corona. 

Takwimu rasmi za karibuni zilizotangazwa na serikali ya Ujerumani zinaonyesha kuwa, hadi sasa watu 194,705 wameambukizwa virusi vya corona nchini humo ambapo 9,026 miongoni mwao wameaga dunia kwa maradhi ya Covid-19. 

Wakati huo huo ripoti zinasema kuwa Marekani imeendelea kushika nafasi ya kwanza duniani kwa kuwa waathirika wengi zaidi virusi vya corona na vilevile idadi kubwa zaidi ya wahanga wa ugonjwa huo.  Utawala wa Rais Donald Trump uunaendelea kukosolewa vikali kwa uzembe na kutowajibika katika kupambana na virusi vya corona.  Watu zaidi ya 128,000 wamefariki dunia nchini Marekani, huku watu milioni 2.5 wakithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo. 



342/