Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Dakta Tedros Adhanom ametoa ripoti yake na kubainisha juu ya matumaini hayo na kuzitolea wito serikali na wananchi kufaya juhudi ili kutokomeza maambukizi ya corona.
Katika ripoti yake hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa WHO ametangaza juu ya uamuzi wa viongozi wa nchi mbalimbal duniani kwa ajili ya kuchukua hatua za kupambana na maambukizi ya virusi vya corona na akakaribisha pia hatua mpya zinazochukuliwa na wananchi kama njia mbili kwa ajili ya kupambana ipasavyo na maambukizi hayo.
Dakta Adhanom ameashiria maelekezo ya Shirika la Afya Duniani kwa nchi mbalimbali kuhusu hatua kama vile kuwatambua mapema watu wenye maambukizi, kutosongamana watu, utumiaji wa barakoa na kunawa mikono mara kwa mara na kuongeza kuwa: serikali mbalimali kwa kutekeleza hatua hizi tajwa zinaweza kuzuia kuongezeka maambukizi ya corona.
Takwimu za WHO zinaonyesha kuwa, hadi sasa watu milioni 20 na 317,272 wameambukizwa corona duniani na wengine 740,291 wameaga dunia kwa maradhi hayo.
342/