16 Septemba 2020 - 14:20
Al-Wifaq ya Bahrain: Makubaliano na utawala haramu wa Israel ni jinai ya kihistoria

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mwafaka wa Kiislamu na Kitaifa nchini Bahrain (Al Wifaq) amesema kuwa, kutiwasaini hati ya mapatano baina ya Bahrain, Imarati na utawala wa Kizayuni wa Israel ni ni jinai ya kihistoria.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sheikh Hussein al-Daihi, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mwafaka wa Kiislamu na Kitaifa nchini Bahrain (Al Wifaq) amebainisha kuwa, tawala za Bahrain na Imarati zimechukua hatua ya kuanzisha uhusiano na utawala ghasibu wa Israel na hivyo kutenda jinai kubwa kwa hatua yao hiyo kwani zimefanya juhudi za kuuhalalisha utawala huo unaotenda jinai kila leo dhidi ya Wapalestina.

Sheikh Hussein al-Daihi, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mwafaka wa Kiislamu na Kitaifa nchini Bahrain (Al-Wifaq) amebainisha kuwa, tawala za Bahrain na Imarati zimechukua hatua ya kuanzisha uhusiano na utawala ghasibu wa Israel na hivyo kutenda jinai kubwa kwa hatua yao hiyo kwani zimefanya juhudi za kuuhalalisha utawala huo unaotenda jinai kila leo dhidi ya Wapalestina.

Kadhalika, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mwafaka wa Kiislamu na Kitaifa nchini Bahrain (Al-Wifaq) amesisitiza kuwa, daima wananchi wa Bahrain watakuwa pamoja na Wapalestina katika harakati zao za mapambano za kupigania ukombozi wa ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.

Katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja tangu Imarati ilipotangaza kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel, utawala wa kiimla na kidikteta wa Bahrain nao umefuata mkumbo huo, ambapo tarehe 11 Septemba, rais wa Marekani alitangaza rasmi kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Bahrain na utawala wa Kizayuni unaoikalia kwa mabavu Palestina. Usaliti huo wa nchi hizo za Kiarabu umelalamikiwa na unaendelea kulalamikiwa vikali.

342/