Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Wabunge hao wameashiria katika taarifa yao uadui wa viongozi wa ukafiri dhidi ya risala yenye nuru ya Uislamu na kutangaza kuwa, katika siku za hivi karibuni walimwengu wameshuhudia jinsi serikali ya Ufaransa inavyounga mkono vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu ambapo jarida moja la nchi hiyo limeonyesha bayana tena kwa jeuri na ufidhuli mkubwa vitendo vyake vya kumvunjia heshima Bwana Mtume SAW.
Taarifa ya Wabunge hao wa Bunge la Iran imeeleza kuwa, ushenzi na ufidhuli huu ambao ni sehemu ya mipango mikubwa michafu yenye njama ya kupunguza kasi ya watu kuingia katika Uislamu nchini Ufaransa.
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imeeleza kuwa, kasi ya wananchi wa Ufaransa kuingia katika Uislamu imeitia kiwewe serikali ya Paris na ndio maana inafanya na kutetea vitendo kama hivi.
Kadhalika Wabunje wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) wamekosoa vikali kuhalalishwa vitendo hivyo kwa kisingizio cha uhuru wa kutoa maoni na kwamba, kufanya hivyo ni dhulma kubwa dhidi ya uhuru.
Jarida la Kifaransa la Charlie Hebdo siku kadhaa zilizopita lilichapisha tena kibonzo kinachomvunjia heshima Mtume Muhammad (SAW).
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alitetea kitendo hicho cha kutusiwa na kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad SAW, hatua ambayo imeibua hasira na ghadhabu za Waislamu katika maeneo yote duniani.
342/