11 Februari 2021 - 12:45
IAEA: Iran imeanza kuzalisha chuma ya urani

Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) umeeleza katika taraifa yake kuwa, Iran imeanza kuzalisha chuma inayotokana na mada ya urani katika kituo chake cha nyuklia cha Isfahan katikati ya Iran.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Wakala wa IAEA umeeleza kuwa, Rafael Grossi Mkurugenzi Mkuu wa wakala huo amewafahamisha wanachama wa IAEA kuhusu matukio ya karibuni kuhusu shughuli za utafiti na ustawi za Iran katika kuzalisha chuma ya urani kama sehemu ya lengo lililotangazwa kwa ajili ya kuzalisha fueli inayohitajika katika kinu chake cha utafiti cha Tehran. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Grossi ameeleza kuwa: Wakala wa IAEA tarehe 8 mwezi huu wa Februari ulithibitisha uzalishaji wa gramu 3.6 za chuma ya urani katika kiwanda cha kuzalisha Fuel Plate (FPFP) katika taasisi ya nguvu za nyuklia ya Isfahan. 

Kazemgharib Abadi Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Taasisi za Kimataifa zenye makao mjini Vienna Austria jana alieleza kuwa, shughuli za utafiti na ustawi za kubuni aina iliyoboreshwa ya fueli kwa ajili ya kinu cha utafiti cha Tehran zimeanza. 

342/