Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Msemaji wa Idara ya Wafungwa nchini Myanmar amesema kuwa, kama kuna mwanaharakati yeyote aliyetiwa mbaroni kuanzia Februari Mosi mwaka huu wakati jeshi lilipotwaa madaraka ya nchi basi atakuwa miongoni mwa walioachiliwa huru.
Hata hivyo baadhi ya ripoti zinasema kuwa, wengi wa walioachiliwa huru ni wale waliofungwa kabla ya matukio ya Februari Mosi.
Aidha taarifa zaidi zinasema kuwa, kuna raia wengi ambao walitiwa mbaroni katika maandamano ya kupinga hatua ya jeshi ya kutwaa madaraka ya nchi ambao hatima yao haijulikani, kwani hawamo katika orodha ya walioachiliwa huru.
Jeshi la Myanmar lilitwaa madaraka ya nchi Februari Mosi mwaka huu baada ya kumkamata Rais wa nchi hiyo, Win Myint na viongozi wengine akiwemo Aung San Suu Kyi, kiongozi wa chama tawala mwenye ushawishi mkubwa, kufuatia siku kadhaa za mivutano nchini humo.
Kisingizio cha jeshi cha kufanya mapinduzi hayo ni madai yake ya kutokea wizi na udanganyifu katika zoezi la uchaguzi wa Bunge wa Novemba mwaka jana (2020), ambapo kwa mujibu wa matokeo, chama tawala cha National League for Democracy (NLD) kinachoongozwa na Aung San Suu Kyi kiliibuka na ushindi.
342/