Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Shirika la habari la Reuters limezinukuu duru kadhaa za kidiplomasia na kiutawala na kuandika: maafisa wa jeshi wa Mali wamemtia mbaroni Rais, Waziri Mkuu na wa Ulinzi wa serikali ya mpito ya nchi hiyo. Wanajeshi wa Mali ambao hawaridhishwi na serikali mpya nchi hiyo iliyotangazwa na mamlaka ya mpito jana Jumatatu waliwapeleka kwa nguvu Rais na Waziri Mkuu katika kambi ya jeshi la Kati; yapata kilomita chache kutoka mji mkuu Bamako.
Afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Mali ambaye hakutaja jina lake amethibitisha kuwa Rais Bah Ndaw wa serikali ya mpito ya Mali na Waziri Mkuu Moctar Ouane wapo katika kambi ya jeshi ya Kati.
342/