Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Duru ya 13 ya uchaguzi wa Rais wa Iran ilifanyika juzi Ijumaa kote nchini na katika nchi 133 za nje kwa ajili ya kumchagua Rais wa nane wa Iran. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran imetangaza kuwa, Sayyid Ibrahim Raisi ameshinda uchaguzi wa rais wa juzi kwa kupata zaidi ya kura milioni 17 na laki tisa.
Shirika la habari la FARS pia limeripoti kuwa, Rais Nicolas Maduro pia ametuma ujumbe kwa wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiwapongeza kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa Rais wa juzi Ijumaa.
Rais Maduro ametoa mkono wa pongezi kwa Sayyid Ibrahim Raisi kwa kuibuka na ushindi katika duru ya 13 ya uchaguzi wa Rais na kueleza kuwa, rais mteule Ibrahim Raisi na wananchi wanamapinduzi wa Iran wanaungwa mkono kikamilifu na Mapinduzi ya Kibolivari ili kupanua umoja wa watu wa nchi mbili kwa ajili ya mapambano ya kutetea haki za raia, heshima na mamlaka ya kujitawala katika siku za usoni kwenye ulimwengu huu wenye migogoro.
342/