Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa taarifa Admeri Hossein Khanzadi Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelakiwa na Admeri Pierre Vandier, Mkuu wa Jeshi la Ufaransa katika Kisiwa cha Réunion.
Admeri Khanzadi yuko Réunion kuhudhuria mkutano wa saba wa majeshi ya majini ya nchi za kandokando ya Bahari ya Hindi maarufu kwa kifupi kama IONS.
Katika mazungumzo yake na Admeri Vandier, Admeri Khanzadi amesema lengo la kushiriki katika kikao hicho ni kubadilishana mawazo. Aidha amesema Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetayarisha kitabu maalumu kuhusiana na oparesheni za IONS.
Réunion ni kisiwa cha Afrika na mkoa wa ng'ambo wa Ufaransa (kwa Kifaransa: département d'outre-mer, au DOM) katika Bahari Hindi. Kisheria hali yake ni sawa na mikoa mingine ya Ufaransa.
Eneo la Bahari ya Hindi na nchi za pwani mwa bahari hiyo zinahesabiwa kuwa na umuhimu mkubwa wa kistratijia. Kwa sasa karibu asilimia 90 ya biashara yote ya dunia inafanyika kupitia njia za baharini. Iran kwa upande wake, ina mpaka mpana na mkubwa wa majini na uchumi wake unategemea sana suala hilo.
Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limekuwa na mchango muhimu katika kudhamini usalama wa Bahari ya Hindi kutokana na kutuma kundi la meli za kivita zinazoshika doria katika maji ya kanda hiyo na ya kimataifa.
Si hayo tu bali Iran imetoa mapendekezo kadhaa katika uwanja huo ikiwa ni pamoja na kuunda kikosi cha pamoja cha nchi za kandokando ya Bahari Hindi kitakachochukua na ukumu la kulinda usalama wa eneo hilo badala ya majeshi nchi zinazotoka mbali zinazodai kulinda amani katika eneo hilo.
342/