Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Fawzi Barhoum, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameeleza kuwa, makundi ya Palestina yameafikiana katika duru zote za mazungumzo hususan ya Cairo Misri kuhusiana na mpango jumuishi wa kitaifa kuhusiana na uchaguzi na kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa Palestina.
Aidha amesema kuwa, cha ajabu ni kwamba, Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amekuwa akiipatia harakati ya Hamas masharti ambayo kimsingi ni yale yale ambayo yamekuwa yakitolewa na utawala haramu wa Israel.
Hayo yanajiri katikka hali ambayo, ushirikiano wa kiusalama wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina na Israel umeendelea kulalamikiwa na wananchi wa Palestina.
Umati mkubwa wa Wapalestina uliandamana juzi katika mji wa Ramallah ulioko kwenye Ufukwe wa Magharibi mwa Mto Jordan kulaani ushirikiano wa kiusalama uliopo kati ya serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Wapalestina wanaaamini kuwa, taasisi za usalama za Mamlaka ya Ndani ya Palestina hazina jukumu jengine isipokuwa kukandamiza hatua yoyote ile ya kitaifa ya muqawama dhidi ya Wazayuni maghasibu, jambo ambalo linaupa fursa utawala wa Kizayuni ya kubomoa nyumba za Wapalestina, kujenga vitongoji vyengine zaidi na kufuta utambulisho wa Wapalestina.
342/