Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ismail Haniya amesema hayo leo na kueleza kwamba, wanachotaka Wapalestina kutoka kwa mataifa ya Kiarabu ambayo yameanzisha uhusiano wa kawaiada na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ni kutupilia mbali makubaliano hayo.
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema bayana kwamba, njama za utawala vamizi wa Israel za kujipenyeneza katika eneo la Asia Magharibi hakuwezi kubadiliisha udiriki na mwamko wa mataifa ya eneo hili.
Ismail Haniya amekosoa vikali hatua ya baadhi ya mataifa ya Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel na kubainisha kwamba, hatua hiyo katu siyo kwa maslahi ya Palestina na Quds.
Itakumbukwa kuwa, Septemba mwaka jana (2020), Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Imarati na Bahrain walisaini mkataba wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel katika hafla iliyofanyika Ikulu ya White House mjini Washington.
Baada ya hapo Sudan na Morocco nazo zikafuata mkumbo huo huo na kutangaza kuanzisha uhusiano na utawala huo haramu, uamuzi ambao umeendelea kulalamikiwa na kulaaniwa na wapenda haki kote ulimwenguni.
Sudan, Morocco na Bahrain zimeendelea kushuhudia maandamano kila leo ya kulaani na kupinga hatua ya nchi zao ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel, wakisema kuwa, hatua hiyo ni khiyana na usaliti mkubwa kwa wananchi wa Palestina wanaofanyiwa unyama wa kila aina na utawala huo kila uchao.
342/