Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika taarifa ya jana Jumamosi, Wizara ya Habari ya Eritrea imevitaja vikwazo hivyo vipya vya Marekani dhidi ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kuwa 'haramu na visivyo vya kimaadili.'
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, hatua hiyo mpya ya Marekani dhidi ya Eritrea kwa mara nyingine tena imedhihirisha sera ghalati na za kiuadui za Marekani, tena kwa kutegemea madai yasiyo na msingi.
Wizara ya Habari ya Eritrea imesisitiza katika taarifa hiyo kuwa, vikwazo hivyo vya upande mmoja na ambavyo vinakanyaga sheria za kimataifa na mamlaka ya kujitawala nchi hiyo ya Kiafrika ni mbinu ya Washington kukwepa uhalisia wa mambo na kulitwisha taifa hilo mzigo wa lawama.
342/