Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ripoti ya shirika hilo iliyotolewa jana Alkhamisi mjini Sana'a imeongeza kuwa, watoto 3,825 wa Yemen wameaga dunia, huku wengine zaidi ya 4,157, tangu Saudia iivamie nchi hiyo jirani yake miaka sita iliyopita.
Ripoti ya shirika la Entesaf imebainisha kuwa, watoto zaidi ya 3000 wa Yemen wanasumbuliwa na magojwa sugu tangu kuzaliwa kwao, huku wengine wapatao 3000 wakihitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo nje ya nchi hiyo haraka iwezekanavyo.
Mwaka jana, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu Yemen, Lise Grande alionya kwamba, ikiwa vita havitomalizwa katika taifa hilo, basi Yemen itaelekea kwenye hali ambayo haitoweza kubadilishwa na kuingia kwenye hatari ya kupoteza kizazi kizima cha watoto nchini humo.
Kufuatia uungaji mkono wa Marekani, Imarati, utawala haramu wa Israel na nchi nyingine kadhaa za Kiarabu, Saudi Arabia iliivamia kijeshi nchi masikini ya Yemen mnamo Machi 2015 na kuiwekea mzingiro wa pande zote wa nchi kavu, anga na majini. Uvamizi wa kijeshi wa Saudia umeisababishia pia nchi masikini ya Yemen uhaba mkubwa wa chakula na dawa.
342/