Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ujumbe muhimu na wenye faida kwa wote imetolewa na Sheikh letu Sheikh Shafi Allah Amhifadhi unaohusiana na kuchunga Haki ya Mwanadamu na kujihadhari na kumdhulumu Mwanadamu kwa namna yoyote ile, hata kama ni kumdhulumu Furaha yake itakuwa ni katika dhulma kubwa, Bali ni katika madhambi makubwa na Mwenyezi Mungu hawapendi kamwe wenye kudhulumu na hilo ameliweka wazi ndani ya Qur'an Tukufu. Sheikh Shafi akieleza ukweli huo amesema:
"Siku zote, ukiona kwamba huwezi kabisa kuingiza furaha katika nyoyo za watu, basi hakikisha pia kwamba huharibu furaha za watu. Miongoni mwa dhulma kubwa unayoweza kuifanya wewe kama Binadamu, ni kujaribu kuharibu furaha na amani iliyopo ndani ya moyo na nafsi ya mtu mwingine".
Your Comment