Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Michael Cohen wakili wa zamani wa Donald Trump amemkosa vikali Donald Trump katika mahojiano aliyofanya na televisheni ya BBC. Cohen amesisitiza kuwa moja ya makosa makubwa aliyoyafanya Trump ni uwongo mkubwa alioeneza kwamba kura ziliibiwa katika uchaguzi wa rais mwaka jana huko Marekani.
Wakili wa zamani wa Trump ameongeza kuwa matokeo ya uchaguzi hayakuchakachuliwa. Amehoji: Uwongo huo mkubwa utachukuliwaje iwapo atashindwa tena katika uchaguzi wa 2024? Michael Cohen ametumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kukiuka sheria katika masuala ya kifedha, kuwalipa pesa wanawake ambao Trump alikuwa na uhusiano nao wa kingono na kuidanganya Kongresi.
Cohen aidha atatumikia kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu iliyosalia. Cohen alikiri kuhusu tuhuma zinazomkabili na tuhuma kubwa zaidi kati ya zote ilihusiana na suala la uchaguzi wa rais wa mwaka 2016 huko Marekani.
342/