Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ripoti kutoka Vienna zinaeleza kuwa pande husika katika mazungumzo hayo zinakaribia kufikia mtazamo wa pamoja. Ali Bagheri Kani, Mkuu wa Timu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mazungumzo na kundi la 4+1 linaloundwa na Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Russia na China huko Vienna Ijumaa usiku alisema kuwa awamu hii ya mazungumzo imekuwa na matokeo mazuri.
Ali Bagheri Kani amebainisha kuwa: upande wa pili umeafiki mitazamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama msingi wa mazungumzo katika hati mbili kuu za rasimu ya mapendekezo ya vikwazo na suala la nyuklia. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa wakati huo huo ameashiria kuwa kusimamisha mazungumzo halikuwa takwa la Iran. Amesema, kasi ya kufikia mapatano inategemea upande wa pili. Amesema upande wa pili umeafiki mitazamo na misimamo ya kimantiki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba mazungumzo ya awamu mpya yanaweza kuwa ya mwisho na huwenda mapatano yakafikiwa karibuni hivi.
Naye Hussein Amir Abdullahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia wiki iliyopita aliwasiliana kwa simu na Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kusema: Moja ya sababu zinazozorotesha mazungumzo hayo ya Vienna ni kukosekana ubunifu wa kivitendo kutoka upande wa Magharibi.
Hatupaswi kusahau kuwa katika kipindi cha baina ya awamu za sita na saba; pande za Ulaya zilitangaza mara kadhaa katika jumbe zao kwamba zina michango na maoni mapya kwa lengo la kusogeza mbele mazungumzo na kupunguza hitilafu za kimitazamo zilizopo. Hata hivyo baada ya kuanza mazungumzo nchi za Ulaya zimedhihirisha na kuchukua misimamo nje ya fremu ya mapatano ya JCPOA. Pande hizo za Ulaya badala ya kuitaka Marekani kukomesha siasa zake za mashinikizo ya eti kiwango cha juu zaidi na vikwazo vilivyo kinyume cha sheria na kuchukua hatua chanya za kufidia hatua zake za huko nyuma, ndio kwanza zinaweka vizuizi na mashinikizo dhidi ya Iran.
Troika ya Ulaya inayoundwa na nchi tatu za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani nchi ambazo ambazo ziko bega kwa bega na Marekani, ina nafasi katika kutia dosari na kuifanya ni yenye mashaka anga ya mazungumzo hayo ya Vienna. Hivi sasa pia Troika hiyo ya Ulaya imetumia kisingizio cha eti muda hautoshi ili kuzidi kuishinikiza Iran iafiki matakwa yake. Kujiri harakati na matukio mbalimbali sambamba na kuanza duru ya saba ya mazungumzo huko Vienna kunaonyesha kuwa kuna upande unaotumia kila hila kujaribu kuvuruga anga ya mazungumzo hayo.

342/