Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Amnesty International imetoa wito huo kwa mnasaba wa kukaribia maadhimisho ya miaka ishirini tangu kuanzishwa jela hiyo ya kutisha ya Guantanamo.
Jela hiyo iko katika kambi ya jeshi la Marekani nchini Cuba na inajulikana kwa mbinu zake za kikatili na zisizo za kibinadamu katika kuwasaili washukiwa.
Wakosoaji wanasema mbinu zinazotumiwa kuwahoji washukiwa katika gereza hilo ni za kikatili sawa na mateso.
Daphne Eviatar, Mkurugenzi wa Usalama wa Mpango wa Haki za Bindamu wa Amnesty International huko Marekani amesema katika taarifa yake kwamba: "Kadiri gereza hilo linavyoendelea kuwepo na kutumika, ndivyo linavyoharibu zaidi sifa ya Marekani katika suala la kulinda haki za binadamu duniani."
Tangu jela ya Guantanamo ilipoanzishwa Januari 12, 2002, takriban watu 780 wameshikiliwa katika jela hiyo na hadi sasa tuhuma za kutenda uhalifu walizobambikiwa bado hazijathibitika.
Wafungwa 39 wangali wanashikiliwa katika jela hiyo, akiwemo Khalid Sheikh Mohammed, anayeshukiwa kupanga mashambulizi ya 9/11 dhidi ya minara miwili pacha ya jengo la Biashara la Kimataifa la mjini New York.
Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, mwaka mwaka 2009 aliamuru kufungwa gereza hilo, lakini alishindwa kufanya hivyo wakati wa uongozi wake.
342/