16 Mei 2022 - 14:35
Iran: Kitendo cha Wazayuni cha kushambulia jeneza la Abu Akleh kimeonesha dhati ya ukatili ya Israel

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kitendo cha wanajeshi wa utawala wa Kizayuni cha kulishambulia jeneza la mwandishi wa Kipalestina, Shireen Abu Akleh kimeonesha sura halisi ya kikatili ya utawala dhalimu wa Israel.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Saeed Khatib Zadeh amesema hayo leo Jumatatu katika mazungumzo yake ya kila wiki na waandishi wa habari na kujibu swali la mwandishi wa habari wa Iran Press kwamba, kuuliwa kigaidi Shireen Abu Akleh, mwandishi wa habari wa televisheni ya al Jazeera huko katika mji mtakatifu wa Quds, yalikuwa ni mauaji ya makusudi yenye malengo maalumu na ni dhihirisho la wazi kabisa la uvunjaji wa haki za binadamu.

Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia amesema, licha ya wanajeshi wa Israel kumuua kikatili mwandishi huyo wa habari, hata mwili wake nao hawakuuhurumia na jinai hiyo inazidi kuonesha sura halisi ya kikatili ya utawala wa Kizayunii. 

Amesema, wale ambao imma kwa woga au kwa manufaa yao binafsi wanaifuata Israel na kushirikiiana na utawala wa Kizayuni wanapaswa kuelewa kuwa, uwepo wa dola hilo pandikizi unazidi kufutika na kuangamia.

Jumatano iliyopita, wanajeshi makatili wa Israel walimpiga risasi kichwani mwandishi wa habari wa televisheni ya al Jazeera ya Qatar wakati alipokwenda kwenye kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Jenin kwa ajili ya kuripoti uvamizi wa wanajeshi hao.

Maziko ya mwandishi huyo yalifanyika siku ya Ijumaa, lakini wanajeshi hao makatili wa Israel walilishambulia jeneza lake kiasi kwamba lilibakia sentimita chache tu kuanguka chini kabisa. Wanajeshi hao madhalimu waliwapiga marungu na mateke waombolezaji waliokuwa wamebeba jeneza hilo na kufanya liwatoke mikononi.

342/