Katika ujumbe aliotuma kupitia ukurasa wake wa Telegram ambapo ametoa tathmini kuhusu matukio yaliyojiri mwaka huu wa 2022, Medvedev amesema "Russia itaendelea kurudisha ardhi yake ".
"Ni Russia ambayo inajenga mfumo wa ulimwengu ujao, na si Marekani au Uingereza au Kiev iliyo kizani." Aidha amesisitiza kuwa "mfumo kama huo wa ulimwengu utajengwa."
Medvedev amebaini kuwa "Russia inapigana peke yake dhidi ya NATO na Magharibi, kwa hivyo kuchora hali hii haiwezi kulinganishwa na siku za nyuma."
Kulingana na Medvedev, Russia inafanya kila iwezalo kuokoa maisha ya watu wake huku ikiendeleza oparesheni za kijeshi.
Medvedev ambaye aliwahi kuwa rais na waziri mkuu wa Russia pia amezungumzia silaha zinazotumiwa na Russia katika operesheni yake maalum ya kijeshi nchini Ukraine na kusema: "Kwa sababu ambazo ziko wazi kwa watu wote wenye busara, Russia bado haijatumia idadi kubwa ya silaha zake vitani. Wala haijalenga maeneo yote ya adui inayoweza kuyalenga nchini Ukraine. Kila kitu kwa wakati wake."
342/