Rais wa Iran amesema hayo hati katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Alexander De Croo, Waziri Mkuu wa Ubelgiji ambapo sambamba na kueleza hamu ya Iran ya kuwa na mahusiano mazuri na ulimwengu yakiwemo mataifa ya Uulaya amebainisha kwamba, endapo taifa fulani litaathirika na taarifa za uongo na za upotoshaji za makundi ya kigaidi na vibaraka na kuamua kuchagua njia ya kukabiliana na Iran, basi litakuwa limedhurika.
Ebrahim Rais ameongeza kuwa, kukosea mahesabu ni matokeo ya taarifa za uongo na zisizo sahihi na kuongeza kwamba, inasikitisha kuona kwamba, baadhi ya mataifa ya Ulaya yanaunga mkono harakati za chuki dhidi ya Uislamu na harakati za kigaidi.
Ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inataka kuona masuala mbalimbali yanapatiwa ufumbuzi kupitia utendaji na ushirikiano wa pamoja.
Rais wa Iran kadhalika ameeleza kwamba, ardhi za Ulaya hazipaswi kuwa chimbuko la njama na vitisho dhidi yya maslahi ya taifa la Iran.
Kwa upande wake Alexander De Croo, Waziri Mkuu wa Ubelgiji ameeleza umuhimu wa kuimarishwa zaidi uhusiano wa nchi yake na Iran katika fremu ya mahusiano makongwe ya kidiplomasia ya miaka 130 ya Tehhran na Brussels.
342/