Serikali mpya ya mpito, inayoundwa mawaziri 21 inajumuisha wanajeshi na raia, na inaongozwa na Waziri Mkuu wa muda Lamine Zeine Ali Mahamane, ambaye pia ataongoza wizara ya uchumi na fedha.
Aliyekuwa mkuu wa wafanyakazi Luteni Jenerali Salifou Mody, anayeonekana kuwa naibu wa Jenerali Tchiani, ameteuliwa kuwa waziri wa ulinzi wa kitaifa.
Kanali Meja Abdourahmane Amadou, ambaye amekuwa akisoma taarifa nyingi kwenye Televisheni ya serikali tangu mapinduzi ya Julai 26, ni waziri wa vijana na michezo.
Tayari jeshi hilo limewateua wakuu wapya wa kijeshi na kuwafuta kazi maafisa wengi wakuu wa serikali waliohudumu katika utawala wa Bazoum.Serikali ya muda ya Nigeria imepuuzilia mbali mwito wa kufanya mazungumzo uliotolewa na Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na Umoja wa Matafa (UN). Wanajeshi hao wa Niger wanasema hawatubali kuburuzwa na kushinikizwa na Wamagharibi wakiongozwa na Marekani na Ufaransa, wanaowataka warejee kambini na wamrejeshe madarakani Rais Bazoum. Hayo yanajiri katika hali ambayo viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi wameitisha mkutano mwingine wa dharura Alkhamisi ya leo kushughulikia mzozo huo wa kisiasa nchini Niger, baada ya viongozi wa kijeshi kupuuza makataa ya kuachia madaraka. ECOWAS iliwataka wanajeshi waliompindua Mohamed Bazoum kumrejesha madarakani rais huyo wa Niger ndani ya siku saba - kipindi ambacho kilimalizika Jumapili iliyopita- au kukabiliwa na uingiliaji kati wa kijeshi ili kurejesha 'utawala wa kikatiba'.
342/