Baada ya vita vya siku 44 vilivyozuka mwaka 2020 kati ya
Armenia na Jamhuri ya Azerbaijan katika eneo la Nagorno-Karabakh, nchi
hizo mbili zilitia saini makubaliano ya kusitisha mapigano kwa
upatanishi wa Russia; na baada ya hapo sehemu kadhaa za eneo hilo
zilikabidhiwa kwa Jamhuri ya Azerbaijan; lakini licha ya kusainiwa
makubaliano ya kusitisha mapigano, uhusiano kati ya nchi hizo mbili
unaendelea kutawaliwa na mivutano huku kila upande ukimtuhumu mwenzake
kuwa anakiuka makubaliano ya usitishaji vita.
Katika muktadha huo, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Seyed Ebrahim Raisi jana Jumamosi alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Armenia, Nikol Pashinyan, ambaye alimtaarifu kuhusu matukio ya hivi karibuni yaliyozuka katika eneo la Caucasus.
Sambamba na kusisitiza tena upinzani mkali wa Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran kwa aina yoyote ya uzushaji mivutano na kubadilishwa mipaka ya
kihistoria ya eneo hili, Rais Raisi alieleza utayarifu wa Iran kama
jirani madhubuti wa kutoa mchango athirifu wa kuzuia kuibuka mapigano
mapya na mabadiliko yoyote katika hali ya jiopolitiki ya eneo.
Seyyid Ebrahim Raisi ametangaza uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran kwa umoja wa ardhi za nchi zote za eneo na kupinga uwepo wa madola
ya kigeni na akaongezea kwa kusema, masuala ya eneo inapasa yatatuliwe
kwa njia ya mazungumzo na nchi zenyewe za eneo, na Tehran iko tayari
kutoa mchango katika kusaidia kutatua masuala kwa njia ya mazungumzo ya
kidiplomasia.
Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan mbali na
kuwasilisha ripoti ya kina kuhusu matukio ya hivi karibuni katika eneo
la Caucasus Kusini na vilevile matukio yanayojiri kwenye medani ya
mivutano katika eneo la Caucasus amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
daima imekuwa ikitoa mchango chanya na athirifu katika kujenga,
kudumisha na kuimarisha amani, utulivu na usalama katika eneo.../
342/