Vyama vya walimu vimesema mazingira duni ya kazi, tafrani nyingi na mishahara duni ni miongoni mwa sababu kuu zilizosababisha walimu kuacha kazi katika nchi 79 duniani.
Kwa mujibu wa Global News, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetangaza kuwa, walimu milioni 44 zaidi wanahitajika ili kufikia lengo la ulimwengu mzima la elimu ya msingi na sekondari ifikapo mwaka 2030, na vilevile walimu wapatao milioni 15 wanahitajika kwa ajili ya eneo la Afrika, kusini mwa Jangwa la Sahara pekee.
Katika ripoti hiyo imebainishwa pia kwamba, Ulaya na nchi za Amerika Kaskazini ziko katika nafasi ya tatu kwa upungufu wa walimu, na walimu milioni nne na laki 800 wanahitajika katika nchi hizo.
UNESCO imeongeza kuwa: takwimu zinaonyesha kwamba ualimu hauchukuliwi kuwa ni kazi ya kuvutia; na kwa sababu hiyo ni vigumu kuvutia vijana kwenye kazi hiyo, na kwa kawaida, walimu wengi huacha kazi katika miaka ya ya mwanzoni tu baada ya kuajiriwa.
Kwa mujibu wa maafisa waandamizi wa UNESCO, taaluma ya ualimu inakabiliwa na hali mbaya kutokana na walimu wengi kuacha kazi katika miaka ya mwanzoni tu baada ya kuajiriwa na kukosekana pia watu wanaoomba ajira ya ualimu katika baadhi ya nchi.../
342/