9 Oktoba 2023 - 19:09
Kushindwa kwa fedheha mipango ya kijasusi ya Netanyahu dhidi ya Hamas

Edward Snowden, afisa wa zamani wa Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani amesema kushindwa kwa fedheha utawala wa Kizayuni katika operesheni ya "Al-Aqsa Storm (Kimbunga cha Al Aqsa) kuwa ni matokeo ya uzembe wa mfumo wa ujasusi wa utawala huo dhidi ya harakati ya Hamas.

Edward Snowden amelikejeli Baraza la Mawaziri lenye misimamo ya kufurutu ada la utawala ghasibu wa Israel na Waziri Mkuu wake Benjamin Netanyahu baada ya kushindwa huko kwa fedheha utawala wa Kizayuni katika oparesheni ya  Kimbunga cha Al Aqsa iliyofanywa na wanamuqawama wa Hamas. Snowden ameashiria kashfa ya ujasusi ya programu ya Pegasus na kuandika: Netanyahu ameunga mkono tasnia ya mabilioni ya dola na kuuza zana za kijasusi kwa madhalimu wanaozitumia kudukua simu za wakosoaji. 

Amesema, programu umetumika dhidi ya wapinzani, wanasheria wa haki za binadamu na hata wanafunzi; lakini imebainika kuwa  mpango umeshindwa kufanya ujasusi dhidi ya Hamas kama ilivyotazamiwa.  

Pegasus ni programu ya kijasusi iliyotengenezwa na Kundi la NSO lenye makao yake makuu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel)  na kuuzwa kwa nchi nyingi, zikiwemo nchi za Kiarabu, na wakati huo huo hutumiwa na serikali kadhaa za Magharibi kuwafanyia ujasusi wapinzani na viongozi mbalimbali. Baraza la Mawaziri la Netanyahu pia liliwafanyia ujasusi  wapinzani na baadhi ya maafisa wa utawala huo.



342/