6 Novemba 2023 - 16:43
Binti wa Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris ajiunga na watetezi wa watu wa Gaza

Binti wa kambo wa Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, amejiunga na safu ya watetezi na waungaji mkono wa watoto wa Gaza wanaoendelea kuuawa kinyama kwa mshambulizi ya Israel inayopewa himaya na kuungwa mkono na Marekani.

Ella Emhoff, binti wa kambo wa Kamala Harris, Makamu wa Rais wa Marekani, amejiunga na kikundi cha kampeni ya watetezi wa watoto wa Ukanda wa Gaza.

Gazeti la New York Post limeripoti kuwa, binti wa kambo wa Makamu wa Rais wa Marekani, Ella Emhoff, amekuwa akikusanya fedha kwa ajili ya Gaza inayoendelea kuushambuliwa vikali kwa silaha zinazotolewa na Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Emhoff, 24, ambaye baba yake ni Myahudi, Douglas Emhoff, anashiriki katika kampeni ya kuchangisha pesa kwenye akaunti yake ya Instagram, inayolenga kutoa msaada wa haraka kwa watoto huko Gaza.

Ripoti zinasema, kampeni hiyo tayari imekusanya zaidi ya dola milioni 7.8 za michango na inasimamiwa na Mfuko wa Msaada wa Watoto wa Palestina, shirika lisilo la kibiashara lililoko Kent, Ohio.

Wawakilishi wa Kongresi ya Marekani wameelezea wasiwasi na upinzani wao dhidi ya kampeni hiyo. 

Van Drew ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Usalama wa Ndani ya Baraza la Wawakilishi la Marekani amesema: Ukweli ni kwamba, nimeshangazwa na suala hili na linatia wasiwasi mkubwa.

Kampeni ya kuwasaidia watoto wa Gaza iliundwa na baadhi ya wananchi wa Marekani, na watoto wanaunda 50% ya washiriki wake.

342/