Chaim Sofer, kiongozi wa harakati ya Uyahudi wa Othodoksi ya Neturei Karta ameyasema hayo katika mahojiano na chaneli ya televisheni ya Russial-Yaum, ambapo sambamba na kuashiria kwamba mashambulio ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Gaza ni mauaji na jinai amesisitiza kuwa, nchi za dunia zinapaswa kuzuia uendelezaji wa jinai hizo.Kiongozi huyo wa Kiyahudi wa madhehebu ya Othodoksi amesisitiza kwa kusema: "tunalaani mauaji ya Gaza, ambayo hadi sasa yamepelekea maelfu ya watu, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto kupoteza maisha yao. Nchi za ulimwengu, hususan Russia na Marekani zinapaswa kutuma jeshi la kimataifa la kwenda kulinda haki za raia wa Palestina na kuzuia kuendelea kwa mauaji haya".
342/