Katika mkondo huo, Mkuu wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Uingereza amelaani kauli hiyo ya Netanyahu akisema kuwa ni hatari.
Ni baada ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu, kutangaza rasmi siku ya Alkhamisi iliyopita kwamba anapinga kuasisiwa taifa huru la Palestina baada ya kumalizika vita vya Gaza. Alidai kuwa ardhi zote zilizo magharibi mwa Mto Jordani zinapaswa kuwa chini ya udhibiti wa usalama serikali ya Israeli.
Mkuu wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Uingereza, Elisha Kearns, ameliambia gazeti la London Standard kwamba Matamshi ya serikali ya Netanyahu yanazusha mifarakano na ni hatari.
Elisha Kearns ameongeza kuwa: "Hatua ya Netanyahu ya kukataa waziwazi kutambua haki za watu wa Palestina inadhoofisha uungaji mkono wa washirika, inawachokoza majirani na kutuweka mbali na amani."
Wakati huo huo, Brendan O'Hara, msemaji wa uhusiano wa kigeni wa Chama cha Kitaifa cha Scotland, amewataka viongozi wa vyama viwili vikuu vya Uingereza kulitambua rasmi taifa huru la Palestina haraka iwezekanavyo.
342/