20 Januari 2024 - 19:14
Jeshi la Israel lateketeza jengo la chuo kikuu cha Palestina lenye athari za kihistoria za miaka 3,000

Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limelitekeza jengo la Chuo Kikuu cha Al-Israa cha Palestina katika Ukanda wa Gaza chenye athari za kale za kihistoria za tangu miaka elfu tatu iliyopita.

Kwa mujibu wa IRNA, uongozi wa Chuo Kikuu cha Al-Israa katika Mji wa Gaza umelaani kubomolewa kwa jengo la chuo hicho kulikofanywa na utawala wa kinyama wa Kizayuni na kutangaza kuwa athari za kale za kihistoria za zaidi ya miaka elfu tatu zilikuwa zimehifadhiwa katika chuo hicho.Chuo Kikuu cha Al-Israa cha Palestina kilianzishwa mwaka 2014 katika mji wa Az-Zahra katika Ukanda wa Gaza.Kwa mujibu wa ripoti ya Kituo cha Habari cha Palestina, askari wa utawala wa Kizayuni wameshambulia pia kwa mizinga magharibi ya mji wa Khan Yunis kusini mwa Ukanda wa Gaza.

342/