23 Januari 2024 - 14:42
UN: Utawala wa Kizayuni wa Israel unatumia njaa kama 'silaha' dhidi ya Wapalestina

Ripota wa Umoja wa Mataifa anasema utawala wa Kizayuni wa Israel unatumia njaa kama silaha dhidi ya watu Wapalestina wa Ukanda wa Gaza ambao wanakabiliwa na mgogoro mkubwa wa chakula baada ya miaka ya vikwazo na vita vya sasa vya maangamizi ya umati vinavyotekelezwa na Israel.

Mtaalamu maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya chakula, Michael Fakhri, amesema kuwa watoto wote walio chini ya umri wa miaka mitano huko Gaza wanakabiliwa na utapiamlo na wako katika hatari ya uharibifu usioweza kurekebishwa kwa ukuaji wao wa kimwili na kiakili.

Fakhri ameiambia televisheni ya Al Jazeera kwamba: "Hatujawahi kuona raia milioni 2.2 wakilazimishwa kukabiliwa na njaa katika kiwango hiki. Hatujawahi kuona kiwango hiki cha njaa kikitumika kama silaha."

Mtaalamu mwingine, Alex De Waal, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Amani Duniani katika Shule ya Sheria na Diplomasia ya Fletcher katika Chuo Kikuu cha Tufts nchini Marekani, ameunga mkono maoni ya Fakhri, akibainisha kuwa hatua za Israel ni sawa na "uhalifu wa kivita wa njaa".

Ameiambia Al Jazeera kwamba kasi na ukubwa wa tatizo la chakula huko Gaza "haijawahi kutokea" katika historia ya sasa.

342/