27 Julai 2024 - 07:23
Mitihani ya kidunia

Katika mtihani wa dunia, maswali yote yamefunuliwa. Sio tu tumeambiwa maswali ya mtihani, lakini pia tumeambiwa jinsi ya kujibu maswali.

Tumefaulu mitihani mingi katika maisha yetu. hatujawahi kamwe kuona maswali ya mitihani tuambiwe kabla ya mtihani.
Lakini ni tofauti kabisa kuhusu mtihani wa dunia.
Katika mtihani wa dunia, maswali yote yamefunuliwa.
Sio tu tumeambiwa maswali ya mtihani, lakini pia tumeambiwa jinsi ya kujibu maswali.

Kwa mfano Imam al-Sadiq (a) anasema, Luqman al-Hakim alimwambia mwanawe:

:إعلم أنك ستسأل غدا إذا وقفت بين يدي الله عز وجل عن أربع
siku ya Qiyama utakaposimama mbele za Mungu, utaulizwa kuhusu maswali manne.
شبابك فيما أبليته
Ulitumiaje ujana wako?
وعمرك فيما أفنيته
Ulimalizaje umri yako?
ومالك مما اكتسبته
mali yako uliipata wapi?
وفيما أنفقته
Na ulitumia mali yako kwa njia gani?


 Inatosha kurejea Qur’ani na Ahadith ili kupata majibu ya maswali haya.

Hivyo, tumeambiwa kuhusu maswali na majibu pia, kwa hivyo itakuwa mbaya sana ikiwa mtu hakuweza kujibu maswali haya.

Chanzo: alanwaralmunirah