Brigedi za Al-Qassam zimesema katika ujumbe huo uliotolewa jana Jumapili kwamba waziri mkuu wa utawala wa KIzayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu, hajali kuhusu hatima ya mateka hao.
Mkanda huo wa video umetolewa baada ya miili sita ya mateka wa Israel kupatikana huko Gaza.
Tawi la kijeshi la Hamas lisema mateka hao sita walikuwa hai kabla ya mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel na walipaswa kuachiliwa huru katika awamu ya kwanza ya makubaliano ya mateka na wafungwa.
Taarifa ya al Qassam imeongeza kuwa: Vikosi vya jeshi la Israel tayari vimeua mateka wengi "kwa makusudi" na kuchukua miili yao.
Al-Qassam imenukuu taarifa ya Netanyahu kuhusu mateka ambapo amesema anafadhilisha jeshi la Israel libaki kwenye Ukanda wa Philadelphi (Mhimili wa Saladin) kuliko kuokoa maisha ya mateka ambao wangali wanashikiliwa katika Ukanda wa Ghaza.
Mapema jana Jumapili, jeshi la Israel lilitangaza kuopoa miili sita ya mateka kutoka kwenye handaki huko Gaza, na hivyo kuzua hasira miongoni mwa Waisraeli dhidi ya utawala wa Netanyahu.
342/