Maelfu ya watu nchini Marekani walikuja katika mitaa ya Manhattan kuonyesha maandamano yao na kumlaani Benjamin Netanyahu, ambaye amekuja New York kuzungumza katika Mkutano Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa.
Gazeti hili liliandika:
Wakati wote wa siku hii, maandamano kadhaa yamefanyika na makubwa zaidi katika mitaa ya Manhattan na kuzuia harakati za magari na watu kuendelea.
Mvutano kati ya maafisa wa Polisi na waandamanaji ulitokea baada ya giza kuingia katika eneo la Upper East Side (kitongoji cha Manhattan), na waandamanaji kumi na wawili walizuiliwa kwa saa kadhaa.
Maandamano hayo yaliandaliwa na vikundi kadhaa vinavyounga mkono Palestina, ikiwemo "Sauti ya Kiyahudi kwa ajili ya Amani".
Kwa kawaida mikusanyiko hiyo ilikuwa ya amani, lakini baada ya kikundi cha waandamanaji kuhama kutoka Kituo Kikuu cha Grand hadi sehemu ya Kaskazini ya jiji, hali ya anga iliwaka (na kubadilika).
Mmoja wa waandamanaji wa kike, aliyekuwa amevalia kitambaa cheusi kichwani na kitambaa kilichofungwa mabegani mwake, alikuwa ameshikilia bango la kuunga mkono amani wakati afisa wa Polisi alipomfunga pingu.