14 Septemba 2025 - 18:52
Kuhukumiwa Myahudi wa Kiyahudi Orthodox nchini Israel kwa shtaka la kushirikiana na Iran

Moja ya majukumu hayo lilikuwa kutuma kifurushi cha vitisho kwa mwakilishi wa Israel katika Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki. Mahakama imesema ingawa Stern hakutekeleza baadhi ya majukumu hayo, lakini kwa sababu alikubali na kuanza kuyafuatilia, ametambuliwa kuwa na hatia

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti kuwa mahakama ya eneo la Yerusalemu imemhukumu Elimelech Stern, rabi kijana mwenye umri wa miaka 22 kutoka mji wa Beit Shemesh, kwa kosa la kushirikiana na afisa wa kigeni na kupokea majukumu kupitia mtandao wa Telegram.

Kwa mujibu wa ripoti hizo, Stern alikuwa akiwahasiliana na mtu aliyejulikana kwa jina la bandia “Anna Elena” na alipewa majukumu kama vile kutuma vifurushi vya vitisho, kuweka mabango mjini Tel Aviv na kupiga picha za kiusalama.

Moja ya majukumu hayo lilikuwa kutuma kifurushi cha vitisho kwa mwakilishi wa Israel katika Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki. Mahakama imesema ingawa Stern hakutekeleza baadhi ya majukumu hayo, lakini kwa sababu alikubali na kuanza kuyafuatilia, ametambuliwa kuwa na hatia.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha