Meja Jenerali Mohammad Baqeri ametoa onyo hilo pambizoni mwa Mazoezi ya 19 ya Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na kusisitiza kuwa: Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu viko katika kilele cha utayari wake na iwapo adui atafanya kosa lolote basi utawala wa Kizayuni (wa Israel) na yeyote atakayeshirikiana na adui hawatobaki salama.
Hayo ni kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA ambalo limeendelea kumnukuu Mkuu wa Majeshi ya Iran akisisitiza kuwa: "Ulinzi wa anga wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu uko kwenye kilele cha utayari wa kukabiliana na kufanya mashambulizi. Makombora (ya Iran) yanaendelea kuzalishwa kwa wingi na kwa ubora wa hali ya juu sana bila ya kusita."
Meja Jenerali Baqeri amesisitiza pia kuwa: "Kushehenezwa Israel silaha za kivita na jinai zake kupewa uungaji mkono wa pande zote na Marekani ili iendelee kufanya mauaji ya watoto na kutishia usalama wa eneo hili si jambo jipya. Unafiki wa Marekani katika kuupa silaha utawala wa Kizayuni unaoua watoto na kufanya mauaji ya halaiki huko Ghaza unazidi kudhihirisha tabia yao chafu zaidi kuliko huko nyuma."
Awamu ya pili ya mazoezi ya 19 ya Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) ambayo ni luteka kubwa zaidi kikosi hicho, ilianza Jumanne kusini magharibi mwa Iran.
342/
