Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano, Trump alipuuzilia mbali uwezekano wa Ukraine kujiunga na muungano wa kijeshi wa Magharibi. "NATO, unaweza kusahau kuhusu hilo," amesema.
"Pengine ilikuwa ni sababu ya jambo hili zima kuanza," amesema, akikiri kuwa kujitanua NATO upande wa mashariki ni moja ya sababu za kuanza kwa vita kati ya Russia na Ukraine.
Haya yanajiri huku televisheni ya CNN ya Marekani ikitangaza kuwa: Washington imejitenga na nchi za Magharibi kuhusu suala la Ukraine, na hili ndilo jambo lililobadilishwa na Donald Trump kuhusu nafasi ya Marekani kimataifa. Ripoti ya CNN imeongeza kuwa, mwelekeo wa kutatanisha wa Trump kwa Putin na kujitenga na Ukraine umevuruga miungano ya zamani na kuanzisha ushindani wa washirika na wapinzani wa Marekani kwa ajili ya kuunda makubaliano ya amani ambayo anakusudia kufanya na Rais wa Russia.
Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, serikali ya Marekani imeitaka Ukraine kukabidhi haki za uchimbaji madini kwa madini adimu ya nchi hiyo kama fidia ya msaada uliotolewa kwa nchi hiyo katika kipindi cha miaka kumi na moja iliyopita. Trump anasema Ukraine inadaiwa na Marekani kiasi cha dola bilioni 500.
Trump alisema jana Jumatano kwamba, atakutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini Washington siku ya Ijumaa ili kutia saini makubaliano kuhusu rasilimali za madini za nchi hiyo.
342/
