22 Machi 2025 - 21:23
Source: Parstoday
Ayatullah Seddiqi: Uwekezaji kwa ajili ya uzalishaji utastawisha nchi

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran ameeleza kuwa, uzalishaji ni mhimili wa ustawi wa maisha ya watu na ni chachu ya maendeleo na ajira na kusema: "Serikali lazima irahisishe njia za kuvutia viitegauchumi na rasilimali za wananchi kwa kutumia wataalamu mahiri."

Katika hotuba za Swala ya Ijumaa mjini Tehran, Ayatullah Kazem Seddiqi ameashiria hatua ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya kuuita mwaka mpya wa 1404 Hijria Shamsia kuwa ni "Mwaka wa Uwekezaji kwa Ajili ya Uzalishaji" na kusema: Kiongozi Muadhamu amechagua jina hilo si kama kaulimbiu tu, kwa sababu kiongozi huyo mwenye hekima hatoi maneno ya kaulimbiu, bali ni hakika na kweli.

Amesema Kiongozi Muadhamu anatoa mwongozi wa wajibu wa serikali na taifa mwanzoni mwa mwaka kama mpango wa ustawi, na yeye ni baba mwenye upendo kwa umma mzima, anayeliombea mema taifa usiku na mchana.

Katika sehemu nyingine ya hotuba za Swala ya Ijumaa ya leo, Ayatullah Kazem Seddiqi amewahimiza Waislamu kuthamini usiku wa Lailatul Qadr na kusema: "Laylat al-Qadr ni usiku ambao Qur'ani iliteremshwa ndani yake na usiku wa kutakabaliwa dua na maombi. Katika usiku huu, lazima tusafishe nyoyo zetu na kujua thamani yake kubwa."

Ayatullah Seddiqi: Uwekezaji kwa ajili ya uzalishaji utastawisha nchi

Imamu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran pia amelaani mauaji yanayoendele katika maeneo mbalimbali ya dunia hususan huko Palestina na kusema kuwa leo tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na mauaji haya yote ya watoto wachanga na umwagaji damu na tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie hifadhi na kinga.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha