22 Machi 2025 - 21:26
Source: Parstoday
Hamas yatoa wito kwa vyombo vya habari kupinga propaganda chafu za Israel

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa wito kwa Waarabu na Wapalestina kushiriki katika mapambano ya vyombo vya habari ili kukabiliana na propaganda na vita vya kisaikolojia vya Israel vyenye lengo la kuvunja irada na azma ya watu wa Palestina.

Hamas imesema katika taarifa yake kwamba: "Utawala Ghasibu wa Israel unaendesha vita vya kipropaganda na kisaikolojia kwa lengo la kuvunja irada na kusimama kidete watu wa Palestina kupitia njia ya kueneza uvumi na habari za uongo."

Hamas imesema, mashambulizi hayo ya kipropaganda ya Israel yanaenda sambamba na taarifa na matamshi ya washirika wake yanayoshambulia chaguo la Muqawama na mapambano ya ukombozi, na kudhoofisha kusimama kidete kwa watu wetu."

Taarifa ya Hamas imeongeza kuwa, "vita vya propaganda vya utawala vamizi vinalenga watu wetu wenye msimamo thabiti na sauti huru zinazowatetea na kutetea chaguo la Muqawama."

Harakati hiyo imetangaza tena kuwa ina imani kwamba watu wa Palestina "wataendelea kuwa imara na kupigania haki zao, hasa chaguo la mapambano ya pande zote ya ukombozi kama njia bora zaidi ya kurejesha ardhi yao na maeneo matakatifu."

Hamas Imetoa wito kwa wataalamu wa vyombo vya habari na wanaharakati kushiriki katika kampeni kubwa zaidi ya vyombo vya habari ya kulitetea taifa la Palestina na mapambano yake ya ukombozi. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha