28 Machi 2025 - 17:36
Source: Parstoday
Cuba: Uhamiaji umekuwa biashara kwa Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba amepinga viza ya kadi ya dhahabu ya kupewa makazi mkabawa wa dola milioni tano ya Marekani, na kuituhumu serikali ya Trump kwa kutumia suala la uhamiaji kama biashara, kwa kuuza nyumba na kuwafukuza wahamiaji haramu.

Bruno Rodriguez ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X akisema kwamba: Tatizo la uhamiaji limekuwa biashara mpya kwa serikali ya Marekani. 

Rodriguez amesisitiza kuwa: Serikali ya Marekani inauza huduma ya ukazi wa kudumu nchini humo kwa gharama ya dola milioni tano huku ikiwafukuza wahamiaji haramu kwa kukiuka haki zao za msingi za binadamu. 

Rais Donald Trump wa Marekani mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu  alitangaza nia yake ya kutoa visa ya "kadi ya dhahabu", ambayo inaruhusu makazi ya kudumu nchini Marekani kwa raia ambao watatoa kiasi cha dola milioni tano.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba mekosoa mfumo wa kibepari wa Marekani ambapo matajiri wana haki za upendeleo. 

Kama alivyoashiria Bruno Rodriguez, Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, viza hii inachukua nafasi ya viza ya wawekezaji ambayo ilienea pakubwa tangu miaka 35 iliyopita. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha