28 Machi 2025 - 17:37
Source: Parstoday
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds

Mnamo mwaka 1979, mara tu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini alitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa siku ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds, akiwa amesimama imara katika kupigania haki za watu wote wanaodhulumiwa ulimwenguni.

Kila mwaka, katika siku hii, maandamano na mikutano mikubwa hufanyika katika nchi tofauti duniani kutangaza mshikamano na watu wanaokandamizwa, hasa watu wa Palestina, ambao wamevumilia jinai na mauaji ya kutisha zaidi katika ulimwengu wa sasa, kwa kipindi cha miezi 16 iliyopita.

Tamko la Imam Khomeini lililenga kuunganisha sauti za watu wanaodhulumiwa duniani kote dhidi ya madhalimu, waovu na wavamizi.

Ulimwengu umejaa dhuluma, na kubwa kuliko yote ni kukaliwa kwa mabavu Palestina kwa zaidi ya miaka 75 na utawala wa kikoloni na unaotenda jinai za kutisha wa Israel.

Utawala huo unaoungwa mkono na nchi za Magharibi, na hasa Marekani, unaendelea kuwachinja bila huruma Wapalestina huko Gaza, wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake. Kufikia sasa, zaidi ya watu 50,000 wameuawa tangu Oktoba 7, 2023, kwa mujibu wa takwimu rasmi. Takwimu zisizo rasmi ziko juu zaidi.

Utawala huu muovu umeharibu karibu hospitali na shule zote za Gaza, pamoja na miundombinu ya kiraia katika ukanda huo uliozingirwa, na kuwaua watoto wasio na hatia, madaktari, waandishi wa habari, wasomi na wanaharakati katika juhudi zake za kishetani za kuangamiza kizazi kizima cha Palestina.

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds

Katika historia ya binadamu, hakuna chombo chochote kilichowahi kuua watoto wasio na hatia kama utawala muovu wa Israel.

Licha ya ukatili huo wa kutisha, lakini watawala wengi wa nchi za Kiarabu wamesaliti kadhia ya Palestina kwa kufungamana na utawala ghasibu wa Israel na waungaji mkono wake wa nchi za Magharibi.

Serikali ya Marekani imefadhili mauaji hayo ya halaiki yanayoendelea hadi sasa kwa mabilioni ya dola na silaha mbalimbali za kisasa kwa ajili ya kuuwezesha utawala huo wa Kizayuni kuendelea kuwaua wanawake na watoto wasio na hatia huko Palestina.

Bunge la Marekani hata lilimpigia makofi Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Kizayuni, ambaye anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa kuendesha mauaji ya kimbari huko Palestina. Onyesho hilo la kutisha la kushajiisha unyama halijawahi kutokea katika historia ya mwanadamu. Muuaji huyo katili alipongezwa na kushangiliwa na wabunge wa Marekani kwa kuua maelfu ya watoto wa Kipalestina pamoja na mateka wa Israel huko Gaza.

Mauaji ya kimbari yanayoendelea Gaza kwa mara nyingine tena yamefichua sura halisi ya ubeberu wa Magharibi na ukatili wake. Propaganda na madai ya kutetea uhuru, haki za binadamu na demokrasia ni mchezo wa kuigiza tu unaokusudiwa kuhadaa na kupotosha fikra za waliowengi duniani.

Wamewanyima Wapalestina uhuru na haki zao kutokana na uovu uliokithiri, ubaguzi wa rangi na ukatili. Ubeberu wa Kimagharibi ni uovu mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu mwanzo wa historia ya mwanadamu.

Hakuna ukatili unaoweza kulinganishwa na kiwango hiki cha unyama. Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kuteketeza mahema ya watu waliokimbia makazi yao na kuwashambulia kwa mabomu wanawake na watoto wasio na hatia wakiwa wamelala.

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds

Ukweli kwamba Wazayuni walifukuzwa katika nchi nyingi walizokwenda katika historia sasa unaeleweka vizuri. Ni wazi kuwa matendo yao maovu ndiyo yalipelekea wafukuzwe. Uovu ni uovu. Mauaji ya kimbari huko Gaza hayana mfano wake katika historia ya mwanadamu. Unyama wa kupindukia unaotekelezwa na wazayuni wasio na huruma dhidi ya watu wasio na hatia hautasawariki.

Kwa zaidi ya wiki tatu sasa, utawala wa kibaguzi wa Israel umezuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza. Unataka kuwaangamiza Wapalestina kwa kutumia njaa kama silaha ya vita.

Madamu Wapalestina hawako huru, hakuna hata mmoja wetu aliye huru. Nelson Mandela, mwanamapambano shupavu wa Afrika Kusini alikuwa sahihi aliposema: "Uhuru wetu haujakamilika bila ya uhuru wa Wapalestina."

Katika Siku hii ya Kimataifa ya Quds, hebu tuthibitishe tena uungaji mkono na mshikamano wetu na watu shupavu wa Palestina katika mapambano yao halali dhidi ya mlowezi-mvamizi, wauaji, wabaguzi wa rangi na utawala haramu wa Israel. Bilas haka hatimaye Palestina itakuwa huru, kutoka mtoni hadi baharini.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha