28 Machi 2025 - 17:39
Source: Parstoday
Kiongozi Muadhamu: Siku ya Quds ya mwaka huu itakuwa ya aina yake

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu yanayofanyika leo Ijumaa ya Machi 28 kote duniani yana umuhimu mkubwa kuliko miaka iliyopita.

Imam Khamenei amesema hayo katika ujumbe wake uliorushwa hewani usiku wa kuamkia leo kwa njia ya televisheni na kusisitiza kuwa: Matembezi ya Siku ya Kimataifa ya Quds siku ya Ijumaa "Mwenyezi Mungu akipenda, yatakuwa mojawapo ya matembezi bora zaidi, adhimu na yenye heshima."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ameeleza bayana kuwa, Siku ya Quds daima ni ishara ya umoja na nguvu ya taifa la Iran.

Ameeleza kuwa, Siku ya Quds pia ni ishara kwamba taifa la Iran liko imara na thabiti katika malengo yake muhimu, ya kisiasa na ya kimsingi, na katu halitaachana na kaulimbiu ya kuiunga mkono Palestina.

Siku ya Kimataifa ya Quds huadhimishwa kila mwaka katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, kubainisha uungaji mkono wa walimwengu kwa Palestina na kupinga kughusubiwa na uvamizi wa Israel katika ardhi za Wapalestina.

Kiongozi Muadhamu: Siku ya Quds ya mwaka huu itakuwa ya aina yake

Ayatullah Ali Khamanei amebainisha kuwa, "Kwa muda wa miaka 46 iliyopita, wananchi wa Iran walioko kwenye mfungo (wa mwezi mtukufu wa Ramadhani) hushiriki katika maandamano ya Siku ya Quds licha ya mazinigira tofauti ya hali ya hewa, huku kukiwa na mahudhurio sio tu katika miji mikubwa bali hata katika miji midogo na vijiji."

Imam Khamenei amesisitiza kuwa, “Mataifa ya dunia yapo upande wetu, wanaotufahamu wako upande wa taifa la Iran, lakini baadhi ya wanasiasa na serikali zinazotupinga wanaeneza propaganda dhidi ya taifa la Iran: wanataka kuonyesha kuwa kuna tofauti na kuna udhaifu."

Kiongozi Muadhamu ameongeza katika hotuba yake kwa taifa la Iran kuwa, "Maandamano yenu ya Siku ya Quds yatakanusha hila zote hizi na taarifa za uwongo." 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha