28 Machi 2025 - 17:47
Source: Parstoday
Rais Putin: Watu wa Magharibi hawaielewi Russia

Rais Vladimir Putin amesema baadhi ya watu katika nchi za Magharibi hawaielewi Russia, lakini amesisitiza kuwa ukweli huo hauwezi kutatiza hata kidogo ustawi na maendeleo ya nchi hiyo.

Rais wa Russia ameyasema hayo wakati wa mkutano wa Bodi ya Usimamizi ya kundi la 'Movement of the First', ambalo ni shirika la Russia la kutetea maslahi ya watoto na vijana.

Putin amesisitiza kuwa, "Kuna watu katika nchi zinazoitwa za Magharibi ambao hawaielewi Russia. Lakini hii haituzuii kuishi na kujiendeleza. Hii inapasa tu kutupa motisha kuongeza idadi ya watu wanaotuelewa na wanataka kuishi nasi kwa amani na urafiki." 

Rais wa Russia ameeleza bayana kuwa, "Lengo kama hilo linaweza kufikiwa tu kwa kufanya kazi kubwa kwa pamoja na kushirikiana hususan na tabaka la vijana."

Amesisitiza kuwa, "Mafanikio yanatungoja katika uga huu ikiwa tutafanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi na vijana, watoto, na mabarobaro, ambao wanaunda msingi wa mustakabali wa nchi na kuthamini nchi hii." 

Putin ameeleza kuwa, Russia inataka kuona watu wengi zaidi duniani wanaielewa Russia na wanafanya kila wawezalo ili kuishi kwa amani.

Amesisitiza kuwa, pamoja na kuwa baadhi ya watu katika nchi za Magharibi hawana ufahamu kuhusu Russia, lakini hilo kamwe halitazuia hata kidogo harakati za ustawi na maendeleo ya nchi hiyo.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha