Katika dikrii aliyotoa leo Jumamosi kwa Makamu wa Rais, Shahram Dabiri, Rais Pezeshkian amesema kwamba, baada ya kukagua ripoti ya safari ya Dabiri katika Nchi ya Kusini, ameamua kumfuta kazi.
Amesema amechukua uamuzi huo kwa kuwa safari za ubadhirifu za maafisa wa serikali, hata kama zinagharamiwa na mapato ya kibinafsi hazikubaliki, kwa kuzingatia matatizo mengi ya kiuchumi yanayowakabili wananchi wa Iran kwa sasa.
"(Safari hizo) hazihalalishiki na hazikubaliki na zinaenda kinyume na mtindo maisha ya chini unaotarajiwa kwa maafisa wa Iran," Rais Pezeshkian amesisitiza.
Dikrii hiyo ya Rais wa Iran imeendelea kusema, "Urafiki [wetu] wa muda mrefu na huduma zako za thamani katika Ofisi ya Makamu wa Rais wa Masuala ya Bunge hazizuii kutolewa kipaumbele kwa uaminifu, uadilifu, na ahadi zilizotolewa kwa watu."
Wakati huo huo, Fatemeh Mohajerani, Msemaji wa Serikali ya Iran amesema kuwa, uamuzi huo wa Rais Pezeshkian unaonyesha kwamba, hana mapatano ya udugu na mtu yeyote, na vigezo vyake pekee ni ufanisi, uadilifu, uaminifu, na kutanguliza mbele maslahi ya umma.
342/
Your Comment