Taarifa iliyotolewa na msemaji wa YAF, Brigedia Jenerali Yahya Saree imesema, operesheni hiyo ya kulipiza kisasi iliyolenga Tel Aviv imetekelezwa kujibu jinai za mauaji ya kimbari zinazoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ghaza na mauaji ya halaiki ya kila siku ya wananchi hao madhulumu yanayofanywa kwa msaada wa Marekani.
Katika hatua nyingine, vikosi vya ulinzi wa anga vya Yemen vimetangaza kuwa vimetungua ndege isiyo na rubani ya Giant Shark F360 iliyokuwa ikiendeshwa na "adui Marekani na Israel" ilipokuwa ikifanya upelelezi katika Mkoa wa kaskazini mwa Yemen wa Sa'daa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ndege hiyo isiyo na rubani imetunguliwa kwa kutumia kombora lililotengenezwa ndani ya Yemen la kutoka ardhini kuelekea angani.Vikosi vya Ulinzi vya Yemen vimetoa mwito pia wa kuchukuliwa hatua za kivitendo, na kuwataka "watu wote wa umma walio huru" kusimama dhidi ya vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendeshwa na Israel dhidi ya Wapalestina, vikitahadharisha pia juu ya hatari ya kutochukua hatua na uwezekano wa kupanuka uvamizi wa utawala wa Kizayuni katika mataifa mengine ya Kiarabu na Kiislamu.
"Matokeo ya kuonyesha ukimya, kutochukua hatua, na kushindwa kutimiza majukumu ya kidini, kimaadili, na ya kibinadamu yatakuwa mabaya kwa wote," imesisitiza taarifa ya YAF.Wakati huohuo Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza imeripoti kuwa idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi kutokana na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa uungaji mkono wa Marekani imeshapindukia 50,609 na wengine zaidi ya 115,000 wamejeruhiwa.../
342/
Your Comment