Philippe Lazzarini, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), ameelezea mashambulizi hayo kuwa ni uvunjaji wa sheria za kimataifa na ametaka uchunguzi huru ufanyike kuhusu mashambulizi hayo.
Lazzarini ametoa matamshi hayo alipokuwa akilaani kulengwa kwa jengo la UNRWA kaskazini mwa Gaza. Shambulio hilo la Jumatano limeua watoto tisa.
Kupitia chapisho katika mtandao wa X, akizungumzia kuhusu jeshi la Israel kulenga jengo la UNRWA katika eneo la Jabalia, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, amesema: “Hata kifusi kimekuwa shabaha Gaza, kwani vikosi vya Israel vilishambulia jengo la UNRWA huko Jabalia, kaskazini mwa Gaza.”
Ameeleza kuwa jengo hilo la UNRWA lililolengwa hapo awali lilitumika kama kituo cha afya na liliharibiwa vibaya mwanzoni mwa mashambulizi.
Lazzarini amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa za awali, jengo hilo lilikuwa linawahifadhi watu 700 wakati wa shambulio, na watoto tisa, wakiwemo watoto wachanga wa wiki mbili tu, walikuwa miongoni mwa waliouawa.
Amesisitiza kuwa Wapalestina waliokoseshwa makazi kutokana na mashambulizi ya Israel huko Gaza hawana pa kwenda, na hata baada ya jengo la UNRWA kushambuliwa, waliokuwa wakitafuta hifadhi humo waliendelea kubaki.
Katika taarifa nyingine, afisa huyo wa UN alibainisha kuwa “tangu kuanza kwa vita, zaidi ya majengo 300 ya UN yameharibiwa au kuangamizwa kabisa, licha ya utoaji wa taarifa za maeneo ya majengo hayo kwa pande zinazohusika.”
Ameongeza kuwa “zaidi ya watu 700 wameuawa wakiwa wanatafuta ulinzi wa UN” wakati wa mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza, akisisitiza kuwa kutojali majengo ya UN, wafanyakazi wake, na shughuli zake ni uvunjaji wa sheria za kimataifa. Lazzarini alitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi huru juu ya mashambulizi hayo dhidi ya majengo ya Umoja wa Mataifa.
Amesema kuwa tangu Oktoba 2023, zaidi ya majengo 300 ya UN yameharibiwa au kuharibiwa kabisa na Israel, na watu zaidi ya 700 wameuawa wakiwa wanatafuta hifadhi chini ya ulinzi wa Umoja wa Mataifa.
342/
Your Comment