27 Aprili 2025 - 22:43
Source: Parstoday
Zelensky: Kombora lililoua raia 12 Kiev lilikuwa na vifaa vilivyotengezwa na makampuni ya silaha ya Marekani

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amedai kuwa vifaa vilivyotengenezwa na makampuni ya Marekani vilipatikana kwenye kombora lililotumiwa kushambulia mji mkuu wa nchi hiyo Kyiv mapema wiki hii na kuua watu 12.

"Kombora ambalo liliua raia Kyiv lilikuwa na vifaa visivyopungua 116 vilivyotengezwa kutoka nchi zingine - na vingi vyao, kwa masikitiko, vilitengenezwa na makampuni ya Marekani," ameandika Zelenskyy kwenye mtandao wa X.

Shambulizi la kombora lililofanywa siku ya Alkhamisi na jeshi la Russia  katika mji mkuu wa Ukraine Kyiv liliua watu 12 na kuwajeruhi wengine 90, huku Ukraine ikidai kuwa kombora lililotumika katika shambulio hilo lilikuwa ni la Korea Kaskazini.

Hata hivyo, si maafisa wa Russia wala Korea Kaskazini ambao wametoa maoni yao kuhusu madai hayo.Rais wa Ukraine ameendelea kueleza: "uchunguzi wa taarifa za kina kuhusu kombora hilo ungali unaendelea. Hata hivyo, tayari imeshabainika kwamba lilikuwa kombora la balestiki la Korea Kaskazini". 

Katika miezi ya karibuni zimekuwa zikitolewa ripoti kwamba wanajeshi wa Korea Kaskazini wanapigana dhidi ya Ukraine katika vita kati ya nchi hiyo na Russia, huku uhusiano wa Pyongyang na Moscow ukizidi kustawi.Zelensky ameongeza kuwa shughuli za utafutaji na uokoaji manusura zilimalizika jana Jumamosi na kwamba zaidi ya watu 30 wangali wamelazwa hospitalini, ikiwa ni pamoja na wale waliojeruhiwa vibaya sana.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha