Waziri wa ulinzi wa Burundi amelitaka jeshi leo kuonesha mshikamano baada ya kushindwa kwa jaribio la mapinduzi wakati majeshi ya usalama yakipambana kuzuia wiki kadhaa za maandamano ya ghasia ya kuipinga serikali.
Mtu mmoja ameuwawa leo katika mapambano na polisi katika mji mkuu Bujumbura, ameeleza mtu aliyeshuhudia , akiwa mhanga wa hivi karibuni kabisa wa ghasia zilizozuka kutokana na juhudi za rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu madarakani, ambapo zaidi ya watu 20 wamefariki.
Waziri wa ulinzi aliyeteuliwa hivi karibuni Emmanuel Ntahonvukiye ametoa wito wa umoja baada ya jaribio hilo la mapinduzi, ambalo lilizimwa na majeshi tiifu baada ya mapigano mitaani kati ya makundi hasimu ndani ya jeshi hilo.
Hali bora ya Burundi kama taifa inategemea maelewano ya jeshi, taarifa ya jeshi imesema, na kuonya kwamba iwapo jeshi litatengana , hali hiyo itasababisha hali kama inayoonekana katika nchi iliyoharibiwa kwa vita ya Somalia.