11 Juni 2015 - 18:14
 Mapambano Ukraine yasababisha vifo vya watu watano

Raia watatu na wanajeshi wawili wa Ukraine wameuawa katika kipindi cha siku moja iliyopita kufuatia mapambano makali kati ya majeshi ya serikali na waasi wanaoungwa mkono na Urusi mashariki ya nchi hiyo.

Raia watatu na wanajeshi wawili wa Ukraine wameuawa katika kipindi cha siku moja iliyopita kufuatia mapambano makali kati ya majeshi ya serikali na waasi wanaoungwa mkono na Urusi mashariki ya nchi hiyo. Wanawake watatu wameripotiwa kuuawa katika jimbo la Donetsk na wanajeshi wawili wameuawa katika jimbo jirani la Luhansk katika mashambulizi ambayo yamewajeruhi pia wanajeshi wengine 13. Waangalizi wa shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya OSCE wamezishutumu pande zote katika mzozo huo kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa Minsk mwezi Februari yanayoitaka serikali na waasi hao kuondoa silaha nzito katika maeneo yaliyotengwa kuwa salama mashariki ya Ukraine.