28 Julai 2015 - 18:12
Obama: usilaumu ni dini ya suluhu

Rais wa jamhuri ya Marekani aliyasema hayo siku ya Jumanne mjini Addis Ababa huku akisisitiza kupambana dhidi ya ugaidi na vikundi vingine ambavyo vinatumia Uislamu katika kufanya vitendo vya kigaidi barani Afrika nakusema Uislamu ni dini ya suluhu na amani.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: ikinukuu kutoka shirika la habari Irna, ripoti kutoka mjini Addis Ababa makao makuu ya umoja wa Afrika: Rais Baraka Obama alipokuwa akiuhutubia umoja huo alisema maana ya Uislamu ni suluhu na amani.
Aidha alisema magaidi na vikundi vyenye msimamo mkali viliopo katika baadhi ya nchi barani Afrika husingizia Dini, Madhehebu na Uislamu vinapokuwa vikifanya mauaji ya watu wasio na hatia, lakini Waafrika wengi wanaoshi katika bara hili wanafahamu kuwa Uislamu ni dini ya suluhu na amani na wala si ukatili na ugaidi. Sisi tunawajibika kupambana na vikundi vyenye msimamo mkali kama Alqaida, Daesh, Al-Shabab na Boko Haram, huku tukiifahamisha  jamii undani wa vikundi hivi, hivyo Sote tunapaswa kuamini kuwa hao ni makatili.
Kadhalika aliongeza kusema kuwa: Waafrika wanapaswa kufahamu kuwa sisi tuko pamoja nao katika kupambana na vikundi vya kigaidi, kwa maana Washington inaunga mkono juhudi za umoja wa Afrika katika kuleta suluhu na amani katika bara la Afrika.
Aidha alipinga suala unyanyasaji wa kijinsia uliopo katika baadhi ya nchi za Afrika akisema: tunapaswa kupambana na unyanyasaji wa kijinsia uliopo majumbani dhidi ya akina mama, kwani nyumba ni sehemu ya amani kwa familia, hivyo basi kama mwanamke atahisi amani ndani ya familia yake bila shaka jamii pia itakuwa na amani, sisi tunapinga vikali unyanyasaji wa kijinsia na tunaamini kuwa wanawake wanapaswa kuwa na mustakabali mwema sambamba na wanaume.
Kwa upande mwingine katika mazungumzo yake pia alisisitiza kuwa na chaguzi za uhuru na haki katika nchi za Kiafrika huku akikosoa tabia za baadhi ya viongozi wa Afrika kutoacha madaraka baada ya kuisha muhula wao ili kuwapisha wengine kushika nyadhifa hizo.
Naye alimalizia kwa kusema kuwa Waafrika wana haki sawa ya kutumia uhuru wao, kwani hiyo ndio asili ya mwanadamu, na sote tunapaswa kuilinda na kuthamini haki hiyo. Ama Pale ambapo viongozi wa Bara la Afrika unapoisha muda wa utawala wao na kutokuwa tayari kutoka madarakani, maana yake ni kuhatarisha demokrasia kitu ambacho kina ishara  mbaya katika mustakabali wa Afrika. 

 
mwisho wa Habari/ 290