3 Agosti 2015 - 19:55
Netanyahu: muafaka wa Vienna yaifunga Israel

Waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel katika madai yake ya hivi karibuni kuhusu muafaka wa nyuklia wa Vienna amesema kuwa kwa makubaliano haya Iran itaweza kuubana utawa wa Israel

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyombo vya habari vya kirusi katika moja ya ripoti zake zaandika kuwa: waziri mkuu wa utawala wa Israel aliyasema hayo katika mkutano alioufanya na waandishi wa habari alisema kuwa: Israel kwa muda wote itaendelea kupinga muafaka wa mpango wa nyuklia wa Iran uliopitishwa mjini Vienna.
Benjamin Netanyahu alisema: kwa kadri tupatapo vielelezo kamili vya makubaliano ya mpango wa nyuklia wa Iran, ndivyo tutashadidisha kupinga makubaliano hayo, kwani makubaliano ya nyuklia ya Iran ni tishio kwetu na kwa mtazamo wetu bora kusingalifikiwa makubaliano yeyote kwa masharti kama yalioko katika muafaka wa Vienna.
Aidha aliendelea kubainisha madai yake yasio na mashiko kwakusema: serikali ya Iran endapo ikafutiwa vikwazo vilivyo wekewa itapata fursa nzuri ya kutengeza silaha za nyuklia, na yawezekana kuwa hivi sasa ameshaanza kutengeza silaha hizo na kwa muda mchache atakamilisha utengezaji wa silaha za nyuklia.
Inasemekana kuwa makubaliano yaliopatikana mjini Vienna mnamo tarehe 14 Julai mwaka huu ambayo ndio yalikuwa mazungumzo ya mwisho wa mazungumzo ya Iran na kikundi cha 5+1, kwamujibu wa makubaliano ya mpango huo wa nyuklia Iran imepewa ruhusa ya kuzalisha nishati ya nyuklia kwaajili ya matumizi yasiokuwa ya kijeshi kama vile kidaktari, kilimo na nishati ya umeme na masuala mengine ya kibinadamu. Waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel muda wote amekuwa mwenye kupinga makubaliano hayo bila ya kufikia tija yeyote.
Benjamin Netanyahu akitapatapa kutafuta kuugwa mkono na mataifa yenye nguvu duniani, hivi karibuni alimpigia simu Rais wa Urusi akikariri madai yake yakupinga muafaka huo, ama Rais wa Urusi pia hakuwa tayari kukubaliana naye hatimaye akatangaza kuunga mkono kwake muafaka wa mpango wa nyuklia wa Iran.
Mwesho wa Habari/290